Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake inaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ndani ya sardabu ya Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru na watumishi wa Ataba tukufu.

Bibi Rajaa Ali Mahadi kiongozi wa idara ya uhusiano katika ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya amesema kuwa, tumezowea kuomboleza kumbukumbu za vifo vya Ahlulbait (a.s) akaongeza kuwa: “Kawaida huwa tunaalika waislamu wote, wafuasi wa Ahlulbait huja kwa wingi kumpa pole Abulfadhil Abbasi kwa kufiwa na mama yake (a.s), majlisi ilikuwa na Mhadhara wa Dini kuhusu historia ya Ummul-Banina (a.s) pamoja na mambo yaliyo mtokea, majlisi hiyo imedumu kwa muda wa saa mbili”.

Akasema: “Tumezingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji, kama sehemu ya kuheshimu maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na masharti ya wizara ya afya kwa ajili ya kulinda usalama wa wahudhuriaji”.

Kumbuka kuwa idara na vituo vya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya vinaendelea kufanya majlisi na harakati zingine katika kukumbuka matukio yanayo husu Ahlulbait (a.s) na kuangazia maeneo muhimu katika historia zao takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: