Program ya kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole kwa kufiwa na mama yake (a.s)

Maoni katika picha
Mji wa Karbala siku ya mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar umejaa huzuni kila mahala, na unapokea watu wengi wanaokuja kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufiwa na mama yake Ummul-Banina (a.s), kutokana na msiba huo idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu limefanya majlisi ya kuomboleza pamoja na igizo lililo onyesha mambo yaliyomtokea Ummul-Banina (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru pamoja na watumishi wa Ataba tukufu.

Bibi Taghrida Tamimi makamo rais wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara ya wahadhiri imezowea kufanya majlisi katika kila kumbukumbu ya kifo cha mtu miongoni mwa Ahlulbait (a.s), huu ni mwaka wa nne mfululizo idara ya wahadhiri inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), majlisi ya mwaka huu imekua tofauti na miaka ya nyuma kwa kuwepo na maonyesho ya igizo lililo kuwa na vipengele vitano (5) katika historia ya mama huyo mtakatifu, vipengele vyote vilikua na mapokeo yanayokubalika, jumla ya watu (25) wameshiriki katika igizo hilo, igizo limekua na athari kubwa kwa wahudhuriaji”.

Akaongeza kuwa: “Washiriki walikuwa ni wakina mama kutoka idara na vituo vya wanawake vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na wizara ya afya yanayo husu kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi yamezingatiwa”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri huzingatia maudhui katika uwasilishaji wa ujumbe wa Ahlulbait (a.s) kwa makundi yote ya jamii na kwa kuzingatia uwezo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: