Mpiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu amepata tuzo mbili katika shindano na maonyesho ya jumuiya ya wapiga picha wa Iraq

Maoni katika picha
Mpiga picha wa kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya bwana Saamir Khalili Ibrahim Alhusseini amepata tuzo mbili kwenye maonyesho ya jumuiya ya wapiga picha wa kiiraq awamu ya arubaini na nne, ambayo wameshiriki wapiga picha (1183) kutoka kila sehemu ya nchi, tuzo ya kwanza ilikuwa ya dhahabu (ISP) na tuzo ya pili ilikuwa ni midani ya Bronze (IAAP) ya rangi moja.

Husseini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kushiriki katika shindano hili na kupata tuzo hizi ni sehemu ya mfululizo wa tuzo walizo pata wapiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, za kitaifa na kimataifa, kutokana na uzowefu na ufundi walio nao, unao wawezesha kushiriki kwenye mashindano haya, bila kusahau msaada mkubwa wanaopewa na viongozi wao”.

Akaongeza kuwa: “Ushindi huu ni tunu kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa sababu unatokana na baraka zake, pia huu sio ushindi wa kwanza kwangu, nimesha shinda mara nyingi kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa”.

Tawi la jumuiya ya wapiga picha katika mkoa wa Karbala lilipata washindi wawili kwenye shindano hilo, akiwemo mpiga picha bwana Saamir Husseini.

Tambua kuwa zawadi aliyopata Husseini sio hiyo peke yake, alikuwa ameshiriki mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa, tuzo hizi ni muendelezo wa tuzo nyingi alizopata siku za nyuma kwenye mashindano tofauti.

Kumbuka kuwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya na watumishi wake wamesha shiriki kwenye mahafali nyingi za kitaifa na kimataifa, na hufanikiwa kupata tuzo kwenye sekta mbalimbali, kutokana na msaada wanaopata pamoja na bidii zao katika utendaji wa majukumu yao na kupeperusha bendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: