Chuo cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Chuo cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), na nafasi yake katika malezi ndani ya ukumbi wa Nasru-Dini Tusi katika kitivo cha udaktari wa meno na kuhudhuriwa na wahadhiri wachuo, watumishi na wanafunzi, wakiongozwa na rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani.

Majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Abdullahi Dujaili, akazungumzia nafasi tukufu ya Ummul-Banina (a.s) na akahimiza kunufaika na mafundisho yake katika maisha yetu ya kila siku, akakumbusha mambo aliyo fanya na jinsi alivyo jitolea katika kuwahudumia Ahlulbait (a.s), na namna alivyo ishi na Imamu katika fikra zake na harakati zake, akawa ni somo kubwa katika maisha kwa namna alivyo jitolea watoto wake wanne kwa ajili ya kumlinda Hussein (a.s).

Akamaliza mhadhara wake kwa kusoma tenzi zinazo husu utukufu wa mama huyo na subira yake na jinsi alivyo jitolea katika kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu, kupitia watoto wake wanne aliowatuma waende kumnusuru Imamu Hussein (a.s), na jinsi alivyo pambana katika kulinda Dini ambayo bani Umayya walikuwa wanaharibu misingi yake, mama huyu anahadhi kubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: