Kwa mara ya kwanza hapa Iraq: Kiwanda cha mbolea cha Khairul-Juud kinatengeneza mbolea kwa ajili ya nchi za kiarabu

Maoni katika picha
Kiwanda cha teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Khairul-Juud, kimetangaza kuzalisha makumi ya tani ya mbolea kwa ajili ya nchi za kiarabu, baada ya bidhaa zake kuonyesha ufanisi na mafanikio makubwa pamoja na kutoa ushindani na kuthibitisha ubora katika nchi za kiarabu na duniani kwa ujumla, hivyo kiwanda hiki kimekua kiwanda cha kwanza hapa Iraq kupeleka mbolea kinazo tengeneza nje ya nchi, na kufanikiwa kurudisha heshima ya viwanda vya Iraq.

Mkuu wa shirika hilo Mhandisi Maitham Bahadeli ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kiwanda cha mbolea cha Khairul-Juud kimepata mafanikio makubwa, kimeonyesha ufanisi wake kwa wakulima wa Iraq kwa kuongeza kiwango cha mavuno, pia bidhaa zake ni rafiki kwa mazingira na salama kwa matumizi ya binaadamu, bidhaa zake zinastahamili misumu yote ya kilimo, nchi mbili za kiarabu ndio zilianza kuchukua bidhaa za kiwanda hicho kisha zikafuatia nchi zingine.

Akaongeza kuwa: “Watumiaji wa mbolea hizo wamethibitisha ubora wake na jinsi zinavyo ongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao tofauti na mbolea walizokua wanatumia kutoka nchi zingine, jambo hili ni sifa nzuri kwa shirika”.

Tambua kuwa kiwanda kina bidhaa za aina nne, aina tatu ni mbolea (Kavu – kimiminika – mapande) na aina ya nne ni madaya ya mimea.

Kumbuka kuwa bidhaa zote zinazo tengenezwa na kiwanda hiki zinapatikana katika maduka ya shirika yaliyopo Karbala na nje ya Karbala, kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za kiwanda zilizopo barabara ya (Karbala – Najafu) mkabala na nguzo namba 1145 au piga simu namba (07801035422) au (07801930125).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: