Muwakilishi wa umoja wa mataifa Karbala amesema kuwa: Katika makumbusho ya Alkafeel tumeona mpangilio mzuri na weledi wa kazi

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha ratiba ya (marafiki wa makumbusho), inayo husisha kukaribisha watu muhimu na wadau wa makumbusho kwa ajili ya kuangalia malikale zake, miongoni mwa wageni walio tembelea makumbusho ni muwakilishi wa umoja wa mataifa katika mkoa wa Karbala Dokta Ali Kamuna.

Ametembelea sehemu za makumbusho akiwa pamoja na rais wa makumbusho hiyo Ustadh Swadiq Laazim, ameangalia malikale na kusikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu malikale hizo, pamoja na shughuli zinazo fanywa na wahudumu wa makumbusho za uhifadhi na utangazaji wa vitu vilivyomo kwenye makumbusho hiyo, hali kadhalika wameongea kuhusu maendeleo ya sekta ya utalii na kazi za makumbusho katika mkoa wa Karbala.

Mwishoni mwa ziara hiyo Dokta Kamuna ameonyesha kufurahishwa na alicho kiona, pamoja na kazi kubwa inayo fanywa katika makumbusho hiyo, akabainisha kuwa: “Katika ziara hii tumeona mpangilio mzuri na umakini wa kazi, kuna weledi mkubwa katika utunzaji wa malikale za makumbusho, tunawatakia mafanikio mema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: