Kukamilika semina ya Quráni kwa wanafunzi wa Dini wasio ongea kiarabu

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaat Afriqiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni, kwa kushirikiana na Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu Ashrafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekamilisha semina ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ya kwanza, inayo husu ufundishaji wa usomaji sahihi wa Quráni tukufu pamoja na hukumu za usomaji na uandishi wake, kwa wanafunzi wa Dini kutoka bara la Afrika katika nchi zisizo ongea lugha ya kiarabu chini ya ratiba ya mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini.

Semina hii ni zao la ushirikiano wa vituo na taasisi za Atabatu Abbasiyya tukufu, imedumu kwa muda wa mwezi mmoja na nusu, wamefundishwa kwa nadhariyya na vitendo, chini ya walimu walio bobea katika sekta hiyo na wenye uzowefu mkubwa.

Semina hiyo imehitimishwa kwa kufanya hafla na kukabidhi vyeti kwa washiriki sambamba na kuwapa zawadi wakufunzi wa semina hiyo mbele ya mkuu wa kituo hicho Shekh Saadi Shimri na kiongozi wa tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu Sayyid Muhandi Almayali.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekua ikifanya miradi mbalimbali ya Quráni inayo lenga makundi tofauti ya watu, miongoni mwa miradi hiyo ni utoaji wa semina za Quráni kwa wanafunzi wa Dini kama hii iliyofanywa katika mkoa wa Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: