Haram takatifu ya Atabatu Askariyya imekuwa mwenyeji wa shughuli za kituo cha Multaqal-Qamaru

Maoni katika picha
Atabatu Askariyya imekuwa mwenyeji wa shughuli za kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, shughuli ya warsha na mihadhara kwa vijana wa Bagdad na Baabil.

Shughuli hizi ni sehemu ya harakati za kituo na moja ya kazi zake, inatarajiwa kuwafikia vijana wa mikoa mingine kupitia Ataba zingine pia, ili kuweza kunufaisha vijana wengi zaidi, na kuwapa malezi ya kiroho kutokea katika malalo hizo takatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho Shekh Harith Daaji aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kuwa: “Kituo cha Multaqal-Qamaru katika mji wa Samaraa Askariyyaini (a.s), ni sehemu mpya miongoni mwa sehemu za kituo inayo tarajiwa kufanikisha malengo yake, tumewasiliana na Atabatu Askariyya takatifu katika kufanikisha ratiba ya shughuli hii, ambayo imeanza kwa kutembelea Maimamu wawili Askariyaini (a.s) na kuwasilishwa mihadhara minne iliyo tolewa na watumishi wa kituoa, mihadhara miwili inasema: (Imamu Mahadi katika mtazamo wa Ahlulbait –a.s-) na miwili (hukumu za kisheria na vyanzo vya dalili)”.

Akabainisha kuwa: “Ziara hii itahusisha Ataba zingine, tunatarajia kutoa huduma za kifikra na kitamaduni kwa washiriki kupitia ratiba hii katika mazingira magumu tunayo pitia kwa sasa”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba imehitimishwa kwa kukutana na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Askariyya Shekh Yusufu Aaidi, amesisitiza kuwa milango ya malalo takatifu ya Askariyyaini (a.s) iko wazi kutoa ushirikiano katika ratiba kama hii, amewatakia mafanikio mema wasimamizi wa ratiba hii, aidha amegawa vyeti vya ushiriki kwa watu wote walioshiri kwenye ratiba hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: