Chuo cha Alkafeel na Al-Ameed vinapokea wanafunzi waliokubaliwa kusoma bule

Maoni katika picha
Chuo cha Alkafeel na Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vimeanza kupokea wanafunzi waliokubaliwa kusoma bule, baada ya kukamilisha usajili kupitia idara zao rasmi za usajili, na kwa mujibu wa muongozo uliowekwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atakatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amekutana na wanafunzi waliokubaliwa akiwa pamoja na rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nurisi Muhammad Dahani na Dokta Muayyad Ghazali kila mmoja kwa wakati wake ndani ya ukumbi wa chuo, akawatakia mwaka mwema wa masomo na akawaomba wafanye kila wawezalo kufanikisha malengo yao, wanafunzi walio pata nafasi hii waweze kuendelea na safari yao ya kutafuta elimu, hali kadhalika marais wa vyuo hivyo wameeleza mpangilio wa masomo na utaratibu wanao fuata.

Tambua kuwa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu inathamini ushirikiano kati ya vyuo binafsi ukiwemo huu wa chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed, pamoja na juhudi ya kuongeza nafasi za bure, kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wetu watukufu na kuwawezesha kufikia ndoto zao kielimu na matarajio yao ya kutumikia jamii.

Kumbuka kuwa wanafunzi wanaopata nafasi hizo ni watoto wa mashahidi na mayatima wanaotambuliwa na vituo rasmi vya mayatima, pamoja na wanafunzi kutoka kwenye familia za watu wenye kipato kidogo wanao tambuliwa na kamati za ustawi wa jamii, na watoto wa watu wanaojitolea katika Hashdu-Shaábi au mwanafunzi mwenyewe awe katika wanaojitolea kuhudumia Hashdu-Shaábi, na wale wenye mahitaji maalum bila kusahau wakazi wa vijijini na wale ambao familia zao zimeambukizwa virusi vya Korona au magonjwa mengine makubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: