Kituo cha turathi za Karbala kinatoa zawadi kwa watafiti wa mambo ya turathi

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimewapa zawadi watafiti wa mambo ya turathi, hususan walio changia kufanikiwa shughuli za kongamano la kimataifa la (turathi za Karbala na nafasi yake katika maktaba za kiislamu).

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Dokta Ihsaan Gharifi amesema kuwa: “lengo la zawadi hizo ni kuwatia moyo watumishi wa kituo na wadau wanaosaidia kufanikiwa kwa makongamano na nadwa mbalimbali zinazo fanywa na kituo hiki, likiwemo kongamano la kimataifa lililofanyika hivi karibuni na kupata mafanikio makubwa, lilikuwa na ujumbe wa Dini na sekula, na kuwashajihisha kuongeza juhudi katika siku zijazo, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali juhudi zao na wawe miongoni mwa waliofaulu siku ya mwisho na atuwafikishe kwa anayo yapenda na kuyaridhia”.

Akafafanua kuwa: “Ofisi ya kituo cha turathi za Karbala imefungua milango ya kushirikiana na wadau wote wa turathi, na kuimarisha mawasiliano, kwa ajili ya kuutumikia mji wa Bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), na kuendeleza turathi za kibinaadamu”.

Zawadi hizo zimetolewa pembezoni ya nadwa iliyofanywa na kituo cha turathi za Karbala chini ya anuani isemayo: (Turathi za Allamah Mirza Jafari bun Ali Naqi Twabatwabai Alhaairiy) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala ni moja ya vituo vinavyo huisha turathi za kibinaadamu katika mji wa bwana wa mashahidi na ndugu yake mbeba bendera (a.s), kipo karibu na watafiti wa turathi kwa ajili ya kuhakikisha zinahuishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: