Raudhatu Ahbaabul-Kafeel imefungua milango yake kwa tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Idara ya Ahbaabul-Kafeel katika Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kupokea watoto wadogo kwa ajili ya kuwafundisha Quráni tukufu, baada ya kusimama ratiba hiyo kwa miezi mingi kutokana na janga la Korona, pamoja na kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi na kulinda usalama wa watoto hao na walimu wao.

Kiongozi wa raudhat bibi Amina Mansuri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Raudhat imefungua milango yake baada ya kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi kwa ajili ya kuzuwia kuenea kwa virusi vya Korona”.

Akabainisha kuwa: “Hakika Raudhat inatumia njia za kisasa katika ufundishaji wake, pamoja na kuhifadhisha watoto juzuu la thelathini kwa hatua mbili (Riyadhul-Atfaal na hatua ya Tamhidi)”.

Kumbuka kuwa Raudhat ilianzishwa mwaka 2014, inapokea wanafunzi wenye umri wa miaka (3 hadi 5), ni darasa maalum la Quráni kwa watoto wa kike tu, jumla wa watoto (190) wamehitimu darara hilo katika awamu sita, bado tunaendelea na darasa hili kwa lengo la kuingiza mapenzi ya Quráni na masomo ya uislamu kwa watoto pamoja na kuwapa malezi ya bora kuanzia utotoni mwao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: