Atabatu Abbasiyya tukufu ilipata nafasi ya kuongea katika kongamano hilo, ujumbe wa Ataba umewasilishwa na Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi kutoka kitengo cha Dini, alianza kwa kutoa pongezi kwa kila aliyeshiriki kwenye shindano hilo na wasimamizi wa kongamano hili tukufu, kisha akasema: “Hakika kuadhimisha mazazi ya bibi Zaharaa (a.s) ni furaha kubwa kwa sababu ni miongoni mwa siri za uwepo na muendelezo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)”.
Akaongeza kuwa: “Hakika kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu inatakiwa kuwe endelevu kwani ndio njia ya kufika kwake, lazima tutumie njia nzuri ya kufikia lengo hilo, moja ya njia hizo ni Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s), hakika wao ni ufunguo wa kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, na mmoja wa watu watakatifu ni bibi Zaharaa (a.s) pamoja na udogo wa umri wake, alikua na mafundisho mengi, tunatakiwa kumuiga na kumfuata”.
Akabainisha kuwa: “Mwenendo wa bibi Zaharaa (a.s) ni muhimu sana, miongoni mwa mambo muhimu katika mafundisho yake ni:
- - Stara na hijabu, alikua kielelezo cha mwanamke wa kiislamu katika vazi la hijabu, hakuwahi kuacha hijabu hata kwenye mazingira magumu zaidi katika maisha yake, aliharibu ujauzito na kuvunjika mbavu yake kwa ajili ya kulinda hijabu.
- - Upande wa ibada, alikua (a.s) anamuabudu Mola wake wakati wa furaha na madhara na alikua anamtegemea katika kila jambo.
- - Utoaji, alitekeleza kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo (Hamtapata wema hadi mtoe mnavyo vipenda) alikua anatoa bila kikomo, wala hahitaji kitu kingine zaidi ya radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu.
- - Dua zake kwa waumini, alikua anawaombea dua sana na kuwaweka mbele zaidi ya nafsi yake, hakika ni mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na burudisho wa jicho lake, maneno kuhusu yeye ni mengi”.
Hafla imepambwa na Quráni tukufu iliyosomwa na Sayyid Haidari Mussawi kisha watu wote wakasimama na kusoma surat Faatihah na kuwarehemu mashahidi watukufu pamoja na kusoma wimbo wa taasisi (Ahdul-Wilaa), halafu ukafuata ujumbe wa taasisi uliowasilishwa na Ustadh Aiman Abdusada Kaadhim, kisha ujumbe wa maktaba ya Marjaa Mkuu Mheshimiwa Sayyid Muhammad Saidi Alhakiim, ulio wasilishwa na Ayatullahi Sayyid Izu-Dini Alhakiim, halafu ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Ahmadi Duri Al-Aamili kutoka Lebanon.
Mwisho wa kongamano ikagawiwa midani ya shukrani kwa waliofanikisha kongamano hili, makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Maitham Zaidi akashiriki kwenye hatua hiyo, halafu ikapigwa kura kumpata mshindi mmoja kati ya watu kumi waliopata nafasi ya kwanza.
Jumla ya (washindi 540) wakiume na wakike waliohifadhi khutuba tukufu ya Fadaki, na dua ya makarimu Akhlaqi ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) wamepewa zawadi.