Kuahirisha kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) awamu ya saba nchini India

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) ambalo hufanywa na Atabatu Abbasiyya kila mwaka nchini India na kushiriki Ataba zingine za Iraq, imetangaza kuahirisha kongamano la awamu ya saba ambalo lilitakiwa kufanyika mwaka huu, huanza mwezi kumi na tatu Rajabu katika kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Kamati imebainisha kuwa: Kutokana na tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kuhakikisha afya na usalama wa wageni tumeamua kuahirisha kongamano hilo mwaka huu.

Kumbuka kuwa kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) hufanywa kwa ajili ya kuadhimisha Ahlulbait (a.s) pamoja na kufundisha utamaduni wao na mwenendo wao uliofundisha dunia uislamu wa kweli, pamoja na kuonyesha nafasi ya Ataba za Iraq katika kufanya makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya nchi, pamoja na kujenga mawasiliano na wapenzi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: