Wito wa kushiriki nadwa zinazo jadili utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha habari na utamaduni, kimetoa wito kwa watafiti na wasomi kutoka ndani na nje ya nchi kushiriki kwenye nadwa itakayo fanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom) kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed chini ya anuani isemayo (fikra na ubunifu) katika sekta ya maktaba na taaluma.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo tajwa Ustadh Hussein Mussawi amesema: “Nadwa hii ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya kupitia vituo vyake na idara mbalimbali, kuhakikisha wanatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 ambayo yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, nadwa hizi ni muendelezo wa mafanikio hayo na msisitizo wa kutekeleza lengo la nne linalo husu elimu kwa wote na kuongeza fursa za masomo, na lengo la tano linahusu aina za jamii na teknolojia ya mawasiliano”.

Akabainisha kuwa: “Kwa yeyote anayependa kushiriki katika nadwa hii atume wazo lake na wasifu wake (cv) kupitia barua pepe ifuatayo info@lccis.net mwisho wa kupokea mawazo na wasifu hizo ni tarehe 14/2”.

Akafafanua kuwa: “Tutaunda kamati ya elimu itakayo simamia kupokea mawazo hayo na kuchagua yatakayo faa kufanywa mada katika nadwa hiyo, itakayo fanywa katika kila wiki mbili ndani ya miezi mitatu, inawezekana mtoa wazo litakalo pasishwa akawa mzungumzaji wa wazo hilo kwenye nadwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: