Rais wa diwani ya wakfu Shia ametembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na katibu mkuu na amepongeza miradi ya Ataba

Maoni katika picha
Rais wa diwani ya wakfu Shia Dokta Haidari Shimri ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), siku ya Jumanne mwezi (19 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na (2 Februari 2021m) na akapokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Dokta Shimri ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Leo tumetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia miradi yake na huduma inazo toa kwa mazuwaru, hili ni moja ya jukumu la diwani Shia la kuunga mkono kazi zinazo fanywa na wadau wake wakuu, ambao ni Ataba na mazaru takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Tunatambua wazi kuwa Atabatu Abbasiyya inatoa huduma bora kwa mazuwaru na wananchi kupitia miradi yake mikubwa na muhimu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, ziara hii itafatiwa na ziara zingine nyingi ili kuimarisha ushirikiano kati ya diwani na Ataba tukufu”.

Akasema: “Mheshimiwa kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na katibu mkuu na wajumbe wa kamati kuu wanamchango mkubwa katika kusimamia miradi hiyo, bila kusahau juhudi za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaofanya kazi kama nyuki”.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema kuwa: “Lengo la ziara hii ni kudumisha mawasiliano kati ya diwani wakfu Shia na Ataba tukufu, na kuangalia jambo linalo weza kufanywa na diwani katika kusaidia miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo hilo ni pongezi kubwa kwa rais wa diwani ya wakfu Shia kwa misaada anayo toa katika kutumikia taifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: