Ardhi imengáa kwa nuru ya Fatuma

Maoni katika picha
Wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama ya leo mwezi (20 Jamadal-Aakhar) ni kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s), mtoto wa Mtume bora na mke wa Imamu wa kwanza msingi wa kizazi kitakatifu cha Mtume (s.a.w.w), hakika yeye ni Kauthara na Nuru inayoangaza, dunia inangáa nuru kwa kuzaliwa kwake.

Kutoka kwa Mufadhil bun Omari anasema: Nilimuuliza Abu Abdillahi Swadiq (a.s): Ilikua vipi kuzaliwa kwa Fatuma (a.s)? akasema: Khadija alipoolewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wanawake wa Maka walimtenga, wakawa hawaingii nyumbani kwake wala hawamsalimii, bi Khadija akawa mpweke, baada ya kupata ujauzito wa Fatuma akawa anazungumzishwa na Fatuma (a.s) akiwa tumboni mwake na kumtaka afanye subira, akawa anaficha jambo hilo kwa Mtume (s.a.w.w), siku moja Mtume akamkuta Khadija anaongea, Mtume akamuuliza unaongea na nani? Akasema: mtoto aliye tumboni mwangu anazizungumzisha na kuniliwaza, akasema: ewe Khadija Jibrilu ameniambia, hakika mtoto huyo ni wa kike na hakika ni mtoto mtakasifu, na Mwenyezi Mungu mtukufu amejalia kizazi changu kitokane na yeye, atatoa Maimamu katika kizazi chake na kuwafanya viongozi katika ardhi baada ya kuisha wahyi.

Khadija aliendelea kuona hali hiyo hadi alipokaribia kujifungua, akawaita wanawake wa kikuraishi na bani Hashim ili waje kumsaidia wakati wa kujifungua, wakamtumia ujumbe usemao: wewe ulituasi, haukukubali kauli zetu, umeolewa na Muhammad yatima wa Abu Twalib fakiri asiyekua na mali, hatuji wala hatusaidii kitu chochote.. bi Khadija (a.s) akasikitishwa na jibu hilo, ghafla wakaingia wanawake wanne warefu kama wanawake wa bani Hashim, akashtuka baada ya kuwaona, mmoja wao akasema: usihuzunike ewe Khadija sisi tumetumwa na Mola wake kuja kwako, na sisi ni dada zako, mimi ni Sara na huyu ni Asia binti Muzaahim naye ni rafiki wako peponi na huyu ni Maryam binti Imraan na huyu ni Kulthum dada wa Mussa bun Imraan, Mwenyezi Mungu ametutuma kwako kuja kukusaidia katika kujifungua, mmoja akakaa upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto na wa tatu akakaa mbele yake na wa nne akakaa nyuma yake, akazaliwa Fatuma (a.s) akiwa msafi mwenye tohara.

Baada ya kuzaliwa nuru yake iliangaza hadi kwenye nyumba za watu wa Maka, haikubaki mashariki wala magharibi ispokua ilifikiwa na nuru hiyo, halafu wakaingia mahuraini kumi kila mmoja akiwa amebeba chombo na birika kutoka peponi, birika likiwa na maji ya kauthar, wakapokewa na wale wanawake aliokua nao na wakamuosha kwa maji ya kauthar, kisha wakatoa vitambaa viwili vyeupe kushinda maziwa na vinanukia kushinda miski na ambari, kimoja wakamfunga na kingine wakamfunika, halafu wakamsemesha Fatuma (a.s) akatamka shahada mbili, akasema: Nashuhudia kuwa hakuna Mola ispokua Allah na hakika baba yangu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na bwana wa Manabii, na hakika mume wangu ni mbora wa mawasii na watoto wangu ni mabwana wa wajukuu, kisha akawasalimia kila mmoja kwa jina lake, viumbe wa mbinguni wakafahamishana kuhusu kuzaliwa kwa Fatuma (a.s), ikawaka nuru kubwa mbinguni ambayo haikuwahi kushuhudiwa kabla ya siku hiyo, wale wanawake wakasema: Ewe Khadija mchukue hakika ni msafi mtakasifu amebarikiwa yeye na kizazi chake.

Akamchukua akiwa ni mwenye furaha kubwa na akaanza kumnyonyesha, Fatuma (a.s) makuzi yake ya siku moja ni sawa na makuzi ya mwezi mmoja kwa watoto wengine, na mwezi mmoja kwake ulikua sawa na mwaka kwa watoto wengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: