Chini ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Fatuma Zaharaa (a.s) iliyo husisha ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi wanaozingatia uvaaji wa Abaa chuoni.
Hafla hiyo imehudhuriwa na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliokuwa na wajumbe wa kamati kuu na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel pamoja na wajumbe wa kamati ya walimu na watumishi wa chuo na wanafunzi.
Mjumbe wa kamati ya uongozi Dokta Abbasi Dida amesema kuwa: “Kuwashajihisha wanafunzi kuvaa Abaa kunalenga kumuiga bibi Zaharaa (a.s) kilele wa kujilina na kujiheshimu”.
Naye rais wa chuo Dokta Nuris Dahani akasema kuwa: “Tunawapongeza kwa kuzaliwa mbora wa wanawake bibi Fatuma Zaharaa (a.s), chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya juhudi kubwa ya kulinda mwenendo wa kiislamu halisi katika jamii zetu na daima kimekuwa kikisimamia safari za wanafunzi kielimu”.
Akasisitiza kuwa: “Ni muhimu kufanyia kazi kwa vitengo mafundisho ya akhlaqi yaliyopo katika sheria ya kiislamu na yaliyo himizwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu, miongoni mwa mafundisho hayo ni kulipenda taifa na kutafuta elimu, mwisho akaushukuru uongozi mkuu wa Ataba kwa kusaidia miradi ya elimu na malezi katika chuo.