Mahudhurio makubwa katika maktaba ya Ummul-Banina kwenye program ya Multaqa-Zaharaa ya kitamaduni na kibunifu

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imeshiriki katika program ya Multaqa-Zaharaa (a.s) iliyo ratibiwa na chuo kikuu cha Zaharaa (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, katika maonyesho ya vitabu yaliyo fanyika kwenye uwanja wa chuo.

Bibi Asmaa Raád Al-Abadi kiongozi wa maktaba ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika huu ni ushiriki mkubwa katika mwaka huu, tumekua na machapisho tofauti ya kidini na kitamaduni, tuna vitabu na majarida mbalimbali, pamoja na machapisho yanayo husu utamaduni wa watoto”.

Akaongeza kuwa: “Maonyesho haya yamefunguliwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na yataendelea kwa muda wa siku mbili, vituo na taasisi nyingi zimeshiriki, kupitia ushiriki huu tunatarajia kufikisha ujumbe wa Atabatu Abbasiyya na malengo yake”.

Akamaliza kwa kusema: “Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) imezowea kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu kila baada ya muda fulani, chini ya usimamizi wa kitengo cha habari na utamaduni, ushiriki wa kwenye program hii umetokana na mualiko tuliopewa, tumeandaa machapisho yanayo endana ya maonyesho haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: