Upanuzi mkubwa kuwahi kushuhudiwa tangu kujengwa kwake karne tatu zilizo pita katika mji wa Karbalaa: Ufunguzi wa mradi wa Maqaam Imamu Mahadi (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Alkhamisi mwezi (21 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (4 Februari 2021m) imefanya ufunguzi wa mradi wa upanuzi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s).

Ufungunzi huo umehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu pamoja na makamo katibu mkuu na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo.

Huu ni upanuzi mkuwa zaidi kufanywa tangu kujengwa kwake karne tatu zilizopita, upanuzi umefanywa kwa umaridadi mkubwa, ujenzi wake unafanana na ule uliofanywa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na unaendana na utukufu wa Maqaam hiyo.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameongea na mtandao wa kimataifa Alkafeel kuhusu mradi huu, amesema kuwa: “Mradi umetekelezwa na shirika la Ardhi takatifu ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa, kwa kuwa sehemu ilipo Maqaam haiwezi kufanyiwa upanuzi pande tatu, imebidi kuifanyia upanuzi upande wa mto wa Husseiniyya, nao ni upande wake wa magharibi, kwa kutumia nguzo ambazo juu yake kumejengwa mfano wa daraja lililobeba jengo hilo, bila kuziba maji au kubadilisha njia yake, eneo lililo panuliwa linakadiriwa kuwa mita (1200), linaunganika na Maqaam kupitia milango maalum, sehemu hiyo inahusisha:

  • - Ukumbi wa wanawake wenye ukubwa wa mita (490).
  • - Ukumbi wa wanaume wenye ukubwa wa mita (310).
  • - Ukumbi wa watoa huduma wenye ukubwa wa mita (150).
  • - Sehemu ya vyoo inaukubwa wa mita (250) takriban.
  • - Tumeweka marumaru sehemu ya chini na kwenye kuta zake, kwenye paa tumeweka madini ya vioo yenye nakshi, mapambo na maandishi mazuri.
  • - Tumetengeneza mlango mkuu wa Maqaam, kwa kuweka mlango mkubwa sehemu iliyokuwa na mlango wa zamani, juu yake kuna sega la pambo lenye upana wa zaidi ya mita nne na pembezoni mwake kuna nguzo zilizo wekwa Kashi-Karbalai.
  • - Tumejenga nguzo ya saa katikati ya Maqaam upande wa mbele, nayo ni moja ya alama zake za wazi, nguzo hiyo inafanana na ile iliyopo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Sehemu ya mbele ya Maqaam imewekwa Kashi-Karbalai yenye nakshi na mapambo ya kiislamu.
  • - Maqaam imewekwa mifumo ya kisasa, kama vile mfumo wa taa, tahadhari, zimamoto, mawasiliano, ulinzi na mingineyo.
  • - Tumetengeneza daraja lenye upana wa mita (7) na urefu wa mita (22) ili kusaidia daraja la zamani na kupunguza msongamano wa mazuwaru.

Kumbuka kuwa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya unapo ingia Karbala upande wa Maqaam ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) nayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu ilichukua jukumu la kuikarabati, kuanzia kubba hadi kwenye kumbi za haram na maeneo mengine, kazi hiyo iliendelea hadi kufikia kufanyiwa upanuzi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: