Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma (a.s): kitengo cha malezi na elimu ya juu kimefungua shule mpya.

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Alkhamisi ya mwezi (21 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (4 Februali 2021h) kimefungua shule mpya ambayo itakua chini ya shule za Al-Ameed, katika kijiji cha Abu Twahiin wilaya ya Husseiniyya mkoani Karbala, kama dalili kuwa janga la Korona halijazuwia kuongeza shule mpya katika uwanja wa shule za Al-Ameed na kuongeza utowaji wa elimu kwa kupokea idadi kubwa ya wanafunzi, na kuweka mazingira mazuri ya usomaji kwa ajili ya kupata matokeo bora.

Ufunguzi wa shule hii umefanyika katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi pamoja na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Swabihi Kaábi, ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shule mpya inaukubwa wa mita (2600) na imejengwa kisasa, kunajumla ya madarasa (24) na maabara nne, sehemu ya kuswalia na ukumbi wa kulia chakula, pia kuna bustani yenye ukubwa wa mita (550) pamoja na sehemu ya michezo mbalimbali, inayo saidia kuwajenga wanafunzi”.

Kumbuka kuwa shule za Al-Ameed, mwaka baada ya mwaka zimekua zikipata maendeleo makubwa kutokana na uzuri wa ratiba zao za masomo, jambo ambalo ndio sababu ya kuwa na kiwango kikubwa cha ufaulu katika mkoa wa Karbala, hakika shule hizo ni kimbilio la familia nyingi za watu wa Karbala, jambo ambalo limepelekea kitengo cha malezi na elimu ya juu kuweka mkakati wa upanuzi wa majengo kwa ajili ya kumudu ongezeko la wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: