Kituo cha turathi za Hilla kinafanya kongamano la tisa la turathi

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya kongamano la tisa la turathi kwa anuani isemayo (Muhammad bun Falahu Masháshai na nakala zake “maneno ya Mahadi”utafiti halisi), mhadhiri wa kongamano hilo ni Dokta Yusufu Shimri, wameshiriki jopo la wasomi na watafiti.

Kiongozi wa idara ya habari Dokta Salaam Jamali amesema kuwa: “Tunaweza kuangalia harakati ya Muhammad bun Falahu Masháshai, kuwa ni muendelezo wa fitna ambazo ni swala la Mahadawiyya (lenye uhusiano na Imamu Mahadi a.f), pamoja na baadhi ya wanachuoni kufumbia macho uhusiano mkubwa wa ibun Fahadi Alhilliy, jambo hili linajieleza lenyewe, harakati ya Masháshai ni muendelezo wa harakati ya Shalmaghani, pia zikaendelezwa na harakati ya Papa baada yake, ni miongoni mwa fikra ambazo hutokea katika Dini zinazo itwa ukengeukaji (Inkhilafaat), kama alivyo elezea maudhui hii balozi Hussein bun Ruuhu pamoja na Shalmaghani na ibun Fahadi Alhilliy na Masháshai, hukumu ya kihistoria ni moja katika harakati za aina hiyo, nazo hufifia na kuibuka baada ya muda mfupi, na kuwa miongoni mwa habari zilizo pita”.

Mwisho ikasomwa kaswida nzuri ya mshairi Alhilliy Swalahu, inayo husu Hilla ya zamani na ya sasa.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Hilla, kilianza na bado kinaendelea kutoa msaada wa kielimu na kitafiti pamoja na harakati za kihistoria zinazo lenga kulinda na kutunza turathi za kiislamu pamoja na kuangazia athari za wasomi wa mji huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: