Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea majeruhi wa Hashdu-Shaábi walio lazwa katika hospitali ya Alkafeel

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea majeruhi wa Hashdu-Shaábi Liwaau/22 walio jeruhiwa wakati wa kuzuwia shambulizi katika mji wa Jazira mkoani Swalahu-Dini ambao wamelezwa hivi sasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel.

Ugeni huo umeongozwa na makamo rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekh Aadil Wakiil, ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii imefanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwa ajili ya kuangalia hali ya majeruhi na kuangalia huduma za afya wanazo pewa, na kuwapa moyo kwa ushujaa walio onyesha wakati wa kuzuwia shambulizi la magaidi wa Daesh”.

Akafafanua kuwa: “Hakika vita baina ya haki na batili bado inaendelea, kuna wanaojaribu kuvunja amani, majemedari hawa wamekuwa macho wakati wote kutibua njama za magaidi na kupambana nao hata kwa kujitolea mashahidi, kutokana na ushujaa wao pamoja na uzalendo walio nao wamefanikiwa kuzuwia mashambulizi mengi ya magaidi, hakika wanawakinga wananchi kwa kutumia vifua vyao, na Mwenyezi Mungu mtukufu amekua mlinzi na msaidizi wao katika kuondoa batili, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi na awaweke peponi pamoja na kuwapa subira watu wa familia zao, na tunamuomba awape afya na kuwaponya haraka majeruhi hawa, aidha tumefikisha salamu za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na dua zao kwa majeruhi”.

Nao majeruhi wakauomba ugeni huo uwafikishie salamu na shukrani zao kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kuwajali huku ambako kunawapa moyo wa kuendelea kujitolea zaidi kwa ajili ya taifa la Iraq na raia wake.

Kumbuka kuwa ziara hii ni sehemu ya mfululizo wa ziara zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya za kutembelea familia za mashahidi na majeruhi katika mikoa yote ya Iraq, kama sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu, na kuthamini kujitolea kwa raia wa Iraq, hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi imechukua jukumu la kuwatibu majeruhi wa askari na Hashdu-Shaábi, na tayali imeshatibu mamia miongoni mwao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: