Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umehudhuria kongamano la wanafunzi katika chuo kikuu cha Kufa

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umehudhuria ufunguzi wa kongamano la wanafunzi la kwanza, litakalo endelea hadi tarehe (18 Februali 2021m), linahusisha vyuo vikuu (56) vya Kufa, litakalo jadili uundwaji wa kikosi cha wanafunzi wenye uwezo wa kufanya mijadala kitaifa na kimataifa.

Ugeni huo umeongozwa na Ustadh Twalaal Biri mshauri mkuu wa kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya pamoja na Dokta Nuris Dahani rais wa chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na muwakilishi wa idara ya uhusiano wa vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano.

Biri akabainisha kuwa: “Kutokana na mualiko uliotumwa Atabatu Abbasiyya tumehudhuria kushiriki uzinduzi wa jambo hili la kitamaduni kwa wanafunzi, linalo endana na matarajio yetu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na vyuo vikuu, na kushiriki katika harakati za kielimu, kongamano hili ni fursa nzuri kwa wanafunzi wa vyuo kushiriki kwenye majadiliano mbalimbali, yatakayo wasaidia kupata uzowefu wa kuongea na kukubali mawazo ya mwingine, kati ya mwanafunzi na mwanafunzi na kati ya walimu”.

Rais wa chuo kikuu cha Kufa Dkt Yaasir Lufta Hasuun kwenye ujumbe wake wa ufunguzi amesisitiza umuhimu wa kusaidia vipaji vya wanafunzi na harakati zao, akasema: “Majadiliano ni miongoni mwa mambo muhimu yanayo wezesha kubadilishana mawazo na tamaduni kijamii na kiuchumi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: