Hatua za uboreshaji wa maabara ya uhandisi wa majengo katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Maabara ya uhandisi wa majengo chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepita katika hatua muhimu za uboreshaji, imefanikiwa kufanya kazi nyingi ndani ya miaka kumi, imeweza kutekeleza majukumu yake kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi vya maabara, vinavyo endana na maendeleo yanayo shuhudiwa.

Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maabara ya majengo ya kihandisi ilianzishwa mwaka (2011m), mwanzoni ilikuwa na jukumu la kupima vifaa vinavyo tumika kwenye miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ufunguzi wake ulitokana na mradi wa upanuzi wa haram tukufu pamoja na miradi mingine, baada ya Ataba kupanua wigo wa miradi ya ujenzi ikawa lazima kuwe na maabara itakayo simamia viwango vya ubora, sambamba na kupima majengo na vifaa vinavyo tumika kwenye ujenzi”.

Akaongeza kuwa: “Maaba imefanyiwa uboreshwaji baada ya kuingia katika ukarabati mkuu mwaka (2015m), na kuwa kituo muhimu kinacho tegemewa kupima miradi mbalimbali, kwani ndio msingi wa kwanza kwenye ujenzi, umefikia hadi kiwango cha kufungua maabara zingine zilizo chini yake, ikiwemo maabara ya: vifaa vya ujenzi, barabara za juu, aina za udongo, lami, na mambo ya kemia”.

Akasisitiza kuwa: “Maabara imefanikiwa kukidhi mahitaji ya miradi yote ya Atabatu Abbasiyya, na kujitosheleza kwenye sekta hiyo muhimu, imesaidia sana kuokoa muda pamoja na kutoa uhakika wa ubora wa miradi ya ujenzi, na sasa imeanza kutoa huduma ya kupima miradi ya ujenzi inayo fanywa na serikali pamoja na watu binafsi ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: