Asali nzuri kwa asilimia %100: kikundi cha wafuga nyuki Alkafeel kinasaidia kuondoa tatizo la upatikanaji wa asali nchini

Maoni katika picha
Kikundi cha wafuga nyuki Alkafeel kimetangaza kuondoa tatizo la upatikanaji wa asali nchini, wanazalisha asali bora kwa vifaa vya kisasa kabisa na wataalamu walio bobea.

Haya yamesemwa na kiongozi wa kikundi cha wafuga nyuki Mhandisi Hassanaini Muhammad, akaongeza kuwa: “Asali tunayo zalisha katika mizinga yetu ni halisi na inaubora wa asilimia %100, yenye aina tofauti, kutokana na kuweka mazingira ya kilimo kinacho endana na uzalishaji wa asali ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kama vile kilimo cha (Kunazi, Mikaratusi, Mauwa na mboga za majani), pamoja na mimea pori ambayo ndio msingi wa utengenezaji wa asali, kwani nyuki hutegemea mauwa kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza asali”.

Akafafanua kuwa: “Asilimia kubwa ya asali inayo zalishwa inatokana na mauwa ya mti wa mkunazi, kwa sababu Atabatu Abbasiyya tukufu inashamba kubwa la mikunazi, lengo la kuandaa shamba hilo ni kwa ajili ya ufugaji wa nyuki kwani asali itoyokanayo na mti huo huwa nzuri sana”.

Akasisitiza kuwa: “Tunazalisha asali halisi isiyo changanywa na kitu chochote na imethibitishwa na maabara, na inauzwa kwa bei nafuu ukilinganisha na asali zingine zilizopo sokoni, na watumiaji wamethibitisha ubora na uzuri wa asali yetu”.

Kumbuka kuwa mradi wa ufugaji nyuki ni sehemu ya miradi ya kilimo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha ni sehemu ya juhudi za kuongeza kipato kupitia miradi ya uchumi ya ndani, pia ni sehemu ya kuhamasisha uboreshaji wa kilimo, pamoja na kuhakikisha mkoa wa Karbala unajitosheleza kwa asali katika hatua ya kwanza, sambamba na kujitosheleza kwenye sekta ya kilimo, chakula na dawa, Ataba tukufu imekamilisha mahitaji yote muhimu yanayo weza kusaidia kujitegemea na kuondokana na utegemeaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, mafanikio yanaongezeka kila siku.

Tambua kuwa kuna vituo vingi vya mauzo, miongoni mwa vituo hivyo ni:

  • - Barabara ya Husseiniyya karibu na kituo cha Baidhaa, vitalu na mizinga ya Alkafeel.
  • - Kituo cha mauzo ya moja kwa moja chini ya kikundi cha wafuga nyuki Alkafeel.. barabara ya Jamhuriyya, karibu na Masrafu-Rafidiin.
  • - Mtaa wa Hussein (a.s), jengo la kibiashara Al-Afaaf, kituo cha kuuza asali na mauwa.
  • - Inapatikana pia kwenye vituo vingi vya Alkafeel vilivyopo mikoani.

Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba ifuatayo (077012446430).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: