Baada ya miaka mitano ya kufanya harakati katika nchi za Ulaya: Maahadi ya Quráni tawi la Landan imetangaza kufunga harakati za Quráni kwa njia ya moja kwa moja (mubashara) huko Ulaya

Maoni katika picha
Baada ya miaka mitano ya ufundishaji mfululizo na kuhudumia waislamu katika sekta ya Quráni, pamoja na utoaji wa mihadhara, semina kwa wanaume na wanawake wenye umri tofauti katika miji tofauti ya Ulaya kama vile: Birmingham, Manchesta, Liidiz, Livapul, Hill, pamoja na mji mkuu Landan, kutokana na janga la Korona na ugumu wa kuwasiliana moja kwa moja na familia za waislamu katika nchi za Ulaya, Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imetangaza kufunga harakati za Quráni za moja kwa moja katika tawi la Landan, kwa wale wanaopenda kuendelea kusoma kwa njia ya mtandao, wawasiliane na Maahadi ya Quráni katika mji mtukufu wa Karbala.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa shukrani nyingi kwa taasisi zote na watu binafsi waliosaidia Maahadi ya Quráni katika nchi za Ulaya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: