Kuanza kusajili wanafunzi katika shule ya Fatuma bint Asadi (a.s) ya Quráni

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua milango ya usajili katika shule ya Fatuma bint Asadi (a.s) ya Quráni katika mwaka wa masomo 1442h, kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Muda wa masomo katika shule hii ni miaka sita, miaka minne ya kwanza ni elimu ya awali na miaka miwili ya kubobea katika masomo ya Quráni, katika kila hatua kuna selebasi maalum, itakayo fundishwa na walimu wakike mahiri, pamoja na masomo ya Quráni pia watafundishwa masomo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Watafundishwa masomo mengi, ikiwa ni pamoja na kusahihisha Usomaji wa Quráni, Hukumu za tajwidi, Ulumul-Quráni, Tafsiri, Balagha, Nahau ya Quráni pamoja na Fiqhi na Aqida”.

Akabainisha kuwa: “Usajili unafanywa kila siku –ispokua Ijumaa- kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane baada ya Adhuhuri, katika majengo ya shule yaliyopo kwenye kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) katika mkoa wa Karbala, mtaa wa Mulhaqu, barabara ya hospitali ya Husseini, karibu na jengo la Swahibu-Zamaan (a.f), mwanafunzi awe na kitambulisho cha uraia au cha makazi na picha mbili ndogo, kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba zifuatazo: (07602338401 – 07732633510)”.

Akasisitiza kuwa: “Katika mazingira ya kawaida masomo yataendeshwa kwa wanafunzi kuhudhuria darasani, lakini kwa sasa kutokana na janga la virusi vya Korona masomo yatatolewa kupitia mitandao ya kijamii, na walengwa ni wasichana wa mkoa wa Karbala peke yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: