Kituo cha maji cha Atabatu Abbasiyya kimeongeza uzalishaji wake lita (elfu 12) kwa saa

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya maji chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameongeza kiwango cha uzalishaji wa maji lita (elfu 12) kwa saa, ili kuziba pengo la upungufu wa maji safi ya kunywa, na kutosheleza mahitaji ya Ataba na mazuwaru wake pamoja na majengo yanayo izunguka, na kuongeza mitambo ya hakiba inayo weza kuwashwa wakati wowote pindi utakapo simama mtambo wowote katika mitambo inayofanya kazi kwa sasa, kutokana na ziada hiyo jumla ya maji yanayo zalishwa kwa saa ni lita (elfu 46).

Kiongozi wa idara ya maji katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Basam Hashimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa idara yetu wameongeza mtambo wa kuzalisha maji (RO) ya ziada kwa ajili ya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kiasi cha lita (12000) kwa saa, na kuongeza kiwango cha maji katika kituo kikuu kinacho lisha haram tukufu na majengo yanayo zunguka haram kwani tunasambaza maji hadi kwa majirani zetu pia”.

Akasisitiza kuwa: “Maji tunayo zalisha yanaubora mkubwa, yamethibitishwa na maabara za kupima ubora wa maji, yametimiza vigezo na sifa zote za maji safi na salama kwa kunywa”.

Kumbuka kuwa miongoni mwa miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni mradi wa maji safi ya kunywa ambao unasaidia kuondoa shida ya maji kwa mazuwaru, pamoja na vituo vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, sawa viwe ndani au nje ya haram, sambamba na kugawa kwenye Ataba zingine, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maji kunaufanya mradi huu kuwa muhimu zaidi, watumishi na mafundi wanaofanya kazi kwenye mradi huu, hufanya marekebisho na uborehaji wa mitambo kila wakati, pamoja na kuleta mitambo mipya inapo hitajika, ili kuhakikisha maji yanaendelea kutoka wakati wote bila kukatika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: