Kukamilisha hatua ya pili ya warsha ya maendeleo ya binaadamu kwa watumishi wa kujitolea katika idara ya kufuatilia adabu za ziara

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kimemaliza hatua ya pili ya warsha ambayo wameshiriki watumishi wa kujitolea katika idara ya kufuatilia adabu za ziara, hii ni warsha ya kuwajengea uwezo watoa huduma wa malalo takatifu.

Kuhusu ukamilishwaji wa hatua ya pili ya warsha hii tumeongea na rais wa kitengo cha maendeleo endelevu Dokta Muhammad Hassan Jaabir, amesema kuwa: “Semina na warsha zinazo fanywa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, zinalenga kuboresha utendaji ndani ya Ataba tukufu, chini ya wakufunzi wenye uzowefu mkubwa katika sekta hiyo”.

Akaongeza kuwa: Idara ya kufuatilia adabu za ziara ni miongoni mwa idara zinazotoa hudumia mazuwaru moja kwa moja, hivyo inaumuhimu wa pekee, ukumbi wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu umekamilisha hatua ya pili ya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi thelathini wa kujitolea kutoka mkoa wa Bagdad, wamefundishwa saa (12) mambo waliyo fundishwa ni pamoja na (diplomasia ya kuongea) na (kuchunga muda).

Washiriki wamesifu umuhimu wa mada walizo fundishwa, na kuahidi kufanyia kazi kwa vitendo mambo yote waliyosoma, wakati wa kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: