Rais wa chuo cha Furaat Ausat na wa chuo cha Dahuku wapo katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu kuimarisha ushirikiano baina yao

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea ugeni wa marais wa vyuo vikuu viwili, Furaat Ausat na Dahuku wakiwa na wasaidizi wao pamoja na wakuu wa vitivo, wageni hao baada ya kumaliza kufanya ziara katika malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamekutana na rais wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Twalaal Biri.

Tumeongea na Ustadh Hussein Shaakir kutoka idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya aliye fuatana nao katika ziara hiyo, amesema kuwa: “Wageni kutoka vyuoni na kwenye vituo vya elimu hutembelea Atabatu Abbasiyya wakati wote ndani ya mwaka, tunauhusiano mzuri kupitia makongamano na harakati mbalimbali ambazo huwa tunazifanya kwa pamoja, kwa faida ya taifa na sekta ya elimu, ujio wa wageni hawa ni ishara ya wazi ya ukaribu wa Ataba ilionao na taasisi za kielimu”.

Akaongeza kuwa: “Wageni wamepokelewa na Ustadh Twalaal Biri rais wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mazungumzo yao wamejadili mambo mengi, ikiwemo miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kilimo, viwanda, elimu na mingineyo, pamoja na huduma za kimatibabu zilizo tolewa wakati wa janga la Korona, na miradi muhimu ya kuwahudumia mazuwaru wa malalo takatifu pamoja na maendeleo yanayo shuhudiwa, wageni wamefurahia ushirikiano uliopo wenye tija kwa pande zote mbili sambamba na kufanya harakati zingine”.

Akabainisha kuwa: “Hali kadhalika wageni hao wametembelea malalo ya Imamu Hussein (a.s) na wamekutana na makamo katibu mkuu Ustadh Afdhalu Shami, ambaye ameeleza harakati zinazo fanywa na Ataba tukufu za utoaji wa huduma na ujenzi”.

Mwisho wa ziara hiyo wageni ukaagwa kama walivyo pokelewa, wakatoa mualiko wa kutembelea vyuo vyao siku zijazo, na wakapongeza harakati na shughuli zinazo fanywa na Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuhudumia mazuwaru na taifa hili kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: