Watumishi wa kitengo kinacho hudumia eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanasaidia katika shughuli za ujenzi wa eneo la mlango wa Bagdad

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wanashiriki kwenye ujenzi unao endelea wa eneo la mlango wa Bagdad, kazi hiyo imepiga hatua kubwa, watumishi hao wamesaidia kuweka lami kwenye barabara inayo elekea katika malalo mbili takatifu, baada ya kumaliza kazi ya kuweka kokoto.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara Mhandisi Alaa Hamza Salmaan, akaongeza kuwa: “Hakika watumishi wetu wanashiriki kwenye kazi ya kutengeneza sehemu za milango ya mji huu mtakatifu, ikiwemo mlango huu wa Bagdad, watumishi wetu wanamchango mkubwa, wameweka lami upande wa kulia na kushoto wa barabara hiyo, katika uneo lenye urefu wa mita (318) tena wametumia vifaa vyenye ubora mkubwa, na kwa kufuata ramani kama ilivyo chorwa”.

Akabainisha kuwa: “Hakika kudumisha usafi katika eneo linalo zunguka Ataba mbili tukufu ni miongoni mwa kazi muhimu wanazo fanya, wamekua wakijitahidi kufanya kila jambo linalo husu kuwatumikia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na wanahakikisha linakua katika hali nzuri”.

Kumbuka kuwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na watumishi wa mji wa Karbala pamoja na sekta zingine, wamekua wakitekeleza miradi mbalimbali ya kuhudumia mazuwaru watukufu, ukiwemo huu wa kukarabati barabara inayo elekea mji mkongwe, amayo husaidia sana kupunguza msongamano katika matembezi ya mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: