Chuo kikuu cha Alkafeel kinatoa wito kwa wasomi wa kushiriki katika kongamano la kielimu awamu ya tatu

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimealika wasomi wa sekula waje kushiriki kwenye kongamano la kielimu na kimataifa awamu ya tatu, linalo tarajiwa kufanyika tarehe (22 - 23 Machi 2021m) katika majengo ya chuo, na walipambe kwa fani mbalimbali za elimu ya uhandisi na udaktari.

Uongozi wa chuo umesema kuwa kongamano hilo litafanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed, hospitali ya rufaa Alkafeel na chuo kikuu cha Malezia (UKM), mada zitatangazwa kupitia majarida ya kimataifa yafuatayo:

  • - Majarida ya fani za kihandisi: Materials Science Forum (CiteScore: 0.7, ISSN:0255-5476) • AIP Conference Proceedings (CiteScore:0.6, ISSN:0094-243X) 2
  • - Majarida ya fani za kidaktari: International Journal of Applied Pharmaceutics (CiteScore: 1.0,ISSN:0975-7058) • International Medical Journal (CiteScore: 0.2, ISSN:1341-2051).

Gharama ya kuandaa mada za kihandisi ni ($125) na mwanafunzi wa masomo ya juu ya mada hizo ni ($100) na mada za kidaktari ni ($300) na wanafunzi wa masomo ya juu wa mada hizo ni ($250).

Kwa wasomi wanaopenda kuandaa tafiti za kongamano hilo waingie katika link zifuatazo na kujaza fomu maalum, kwa tafiti za kihandisi ingia link hii: https://conference.alkafeel.edu.iq/Visitors/Reviwer/Science
na mada za kidaktari ingia link ifuatayo:

https://conference.alkafeel.edu.iq/Visitors/ReviwerPh/Medical

tambua kuwa wasomi watakao andaa mada wataandikwa kwenye kitabu kinacho tolewa na chuo kikuu kuwa wamefanya tafiti za kielimu.

Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa maalum wa kongamano, kwa fani za kihandisi fungua link hii: https://conference.alkafeel.edu.iq
na fani za kidaktari fungua link ifuatayo: https://conference.alkafeel.edu.iq/Pharmacy
au piga simu kwa namba zifuatazo (whatsap): 0774000027 – 07808006002.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: