Kukamilika maandalizi ya awamu ya saba ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la wanawake

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la wanawake, limetangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kiufundi na kimkakati kwa ajili ya awamu ya saba, litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) kilele cha utakatifu na haki ishindayo) litakalo fanyika mwezi mosi Rajabu (1442h) sawa na tarehe (14 Februali 2021m).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyasiri amesema: “Tunatarajia awamu hii itakua muendelezo wa mafanikio ya awamu zilizo tangulia, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, kamati imekamilisha kupanga mada za kihauza na kisekula zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo kwa mujibu wa ratiba, na ambazo zinahusu historia na mwenendo wa Imamu Baaqir (a.s) sambamba na malengo ya kongamano”.

Akaongeza kuwa: “Kamati ya maandalizi ya mwaka huu imejaalia kongamono hilo kutosheka na maadhimisho ya miaka kumi tangu kufunguliwa kwa moja ya vituo muhimu katika maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, nacho ni kituo cha kukarabati nakala-kale, kutakua pea na maonyesho madogo na yataelezwa mafanikio yaliyo patikana tangu kuanzishwa kwake, maonyesho hayo yatafanyiwa katika eneo la kituo pamoja na kutembelea vitengo vyake”.

Akasema: “Watu watahudhuria kwenye kongamano hilo, kutakuwa na idadi maalum ya washiriki, pia litarushwa mubashara kupitia mtandao wa Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na mitandao mingine ya mawasiliano ya kijamii pia itarusha mubashara ili kutoa nafasi kwa watu kufuatilia kongamano wakiwa mbali”.

Kuhusu ratiba ya kongamano akasema kuwa: “Kongamano litafunguliwa saa tatu na nusu asubuhi siku ya Jumapili, kutakuwa na ujumbe wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na ujumbe kutoka kwa wageni wa kongamano na kaswida ya mashairi ya umuud, baada ya hapo vitaanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti za kihauza na kisekula, na mwisho utakuwa ni ujumbe wa kamati ya maandalizi na maazimio halafu wahudhuriaji watapewa vyeti vya ushiriki”.

Kumbuka kuwa kongamano hilo linafanywa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu (Baaqir a.s) na kwa lengo la kutunza turathi za Ahlulbait (a.s) na kuzipa umuhimu zaidi, kwani turathi hizo zimejaa misingi bora ya kibinaadamu ambayo inahitajiwa na kila mtu duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: