Kituo cha taaluma na uendelezaji wa vipaji chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeshiriki katika semina ya kusimamia miradi mjini Karbala, jumla ya watumishi 47 wa vituo vya malezi na shule wameshiriki kwenye semina hiyo kupitia jukwaa la (Google Classroom), ambapo wamefundishwa njia za ufundishaji kwa kutumia mitandao.
Ustadh Wasaam Khuzaai kupitia mihadhara aliyo toa kwenye semina hiyo kwa muda wa siku nne ndani ya ukumbi wa Asbaat Alwaarith chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, ameongea njia tofauti na utendaji wa kila moja, namna ya kuandaa na kuifanyia kazi wakati wa ufundishaji, pamoja na namna ya kuandaa mitihani ya wanafunzi na usahihishaji kwa njia ya mkono na mtandao, pamoja na namna ya kutumia ukurasa wa mtandao na kubadili lugha ikiwa ni pamoja na kutengeneza ukurasa wa alama za matokeo ya mitihani, akafundisha kiwango cha ushiriki wa usomaji na jinsi ya kuandika mitihani, mihadhara yake imepambwa na maswali na maoni kutoka kwa washiriki yaliyo lenga kujua namna ya kutatua changamoto zinazo weza kujitokeza.
Mkuu wa idara ya usimamizi wa kihandisi Ustadh Hamza Abdulhussein ameongea kuhusu mada walizo fundishwa washiriki na namna walivyo toa ushirikiano, amesema: “Kutakuwa na mkutano mwingine kwa ajili ya kuweka mkakati wa kuwafundisha watumishi waliobaki, tunampango wa kuendelea kushirikiana na Ataba mbili takatifu na kuandaa utaratibu wa kutoa elimu masafa, na kuufanya kuwa utaratibu wa kudumu sio wakati wa janga la (Korona) peke yake”.