Muonekano wa furaha umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu Baaqir na mjukuu wake Alhaadi (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi wa Rajabu umeingia ukiwa na kumbukumbu za mazazi matukufu, furaha imetanda katika Atabatu Abbasiyya kutokana na kuingia mwezi huu, na kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya ikitanguliwa na Imamu Muhammad Baaqir (a.s), ambaye alizaliwa mwezi mosi Rajabu, halafu anafuata mjukuu wake Imamu Ali Alhaadi (a.s) aliye zaliwa tarehe mbili ndani ya mwezi huu mtukufu.

Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa kwa mabango yaliyo andikwa maneno ya kuonyesha utii kwa watukufu hao, na kuta zake zimepambwa kwa taa za rangi pamoja na mauwa yaliyo wekwa sehemu tofauti ndani ya haram tukufu.

Muonekano wa hafla haupo ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) peke yake, bali upo hadi nje yake, na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, hadi kwenye malalo ya bwana wa vijana wa peponi Abu Abdillahi (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha kumbukumbu hii tukufu, imejaa vipengele vingi kutokana na mazingira yalivyo kwa sasa, ikiwa ni pamoja na kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya saba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: