Mwezi mosi Rajabu dunia ilinawirika kwa kuzaliwa Imamu Muhammad Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi mosi Rajabu mwaka wa 57h, alizaliwa Imamu Muhammad Baaqir aliye bashiriwa na Mtume (s.a.w.w) kabla ya kuzaliwa kwake, watu wa nyumba ya Mtume (a.s) walikua wanamsubiri kwa hamu kubwa, kwa sababu ni katika Maimamu wa waislamu waliotajwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa ni viongozi wa umma na akawasifu kuwa wanahekima, alizaliwa katika mji wa Madina kabla ya kuuwawa babu yake Imamu Hussein (a.s) kwa miaka mitatu, na inasemekana kwa miaka minne.

Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) ndiye Imamu wa kwanza kutokana na maimamu wawili matakasifu (maasumina), baba yake ni Imamu Ali Zainul-Aabidina mtoto wa Imamu Hussein mtoto wa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), hiyo ndio nasaba yake upande wa baba, amma upande wa mama, mama yake ni Fatuma mtoto wa Imamu Hassan bun Ali bun Abu Twalib (a.s), alikua anaitwa (Ummu Abdillahi), alikua mbora wa wanawake wa bani Hashim, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikua anamwita Swidiiqah, Imamu Abu Abdllahi Swadiq anasema: (Alikua Swidiiqah hakuwahi kupatikana katika kizazi cha Hassan mfano wake), yatosha fahari kwake kuwa anatokana na mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na amekulia katika nyumba alizo idhinisha Mwenyezi Mungu kutajwa jina lake, miguu yake mitakatifu ndio iliyomlea Imamu Baaqir (a.s).

Shekh (r.a) amepokea kutoka kwa Amru bun Shimri, anasema: Nilimuuliza Jaabir bun Yazidi Jaáfii kuwa: Kwa nini Baaqir ameitwa jina hilo? Akasema: kwa sababu aliharakia kupata elimu kubwa na kuionyesha.

Alinihadithia Jaabir bun Abdillahi Answari kuwa alimsikia Mtume (s.a.w.w) anasema: Ewe Jaabir hakika utabaki hai hadi utakutana na mtoto wangu Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib anaye julikana katika Taurati kwa jina la Baaqir, utakapo kutana naye mfikishie salamu zangu, Jaabir akakutana naye katika moja ya nyumba za Madina, akamuuliza: Ewe kijana ni nani wewe? Akasema: mimi ni Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Jaabir akasema: ewe kijana njoo akaenda: kisha akasema: rudi akarudi, akasema: Naapa kwa Mola wa Alkaaba, kisha akasema: ewe mwanangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anakutolea salamu: akasema: amani iwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu madam mbingu na ardhi vipo, na kwako ewe Jaabir kwa kufikisha salam, Jaabir akasema: ewe Baaqir, wewe ni Baaqir wa kweli, wewe ndiye utakaepata elimu haraka.

Kisha Jaabir akawa anaenda anakaa mbele yake na anafundishwa, mambo ambayo alikua anakosea au anasahau kama alivyo ambiwa na Mtume (s.a.w.w) Imamu akawa anamkumbusha na kumuelekeza, Jaabir akawa anasema: ewe Baaqir, ewe Baaqir, ewe Baaqir, nashuhudia mbele ya Mwenyezi Mungu hakika wewe umepewa hekima (elimu) ukiwa mdogo.

Katika kitabu cha Tadhkirah-Sibtu ibun Jauzi kimeandika kuwa: aliitwa Baaqir kutokana na wingi wa kusujudu, paji la uso wake lilifanya haraka kusujudu na inasemekana ni kutokana na ukubwa wa elimu yake.

Alisifika kwa kuwa na maneno mazuri pamoja na hoja za nguvu katika mijadala ya Fiqhi, Aqida na hukumu za sharia tukufu, alikua anafanya vikao na wanachuoni wa zama yake, waliokua wanamfuata kumuuliza maswali na kunufaika nae (a.s), Imamu Baaqir (a.s) aliishi katika mji wa Madina na alikuwa anafundisha umma wa kiislamu, na kusimamia mbegu ya wema iliyo pandwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na kutunzwa na Imamu Ali kisha maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s), kisha baba yake Ali bun Hussein (a.s).

Imamu Baaqir (a.s) aliishi na babu yake Imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na zaidi na alishuhudia vita ya Karbala, kisha akaishi na baba yake Sajjaad (a.s) miaka thelathini na nane akichota utukufu kutoka kwake, na muda wa uimamu wake unakaribia miaka ishirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: