Kuzaliwa kwa hoja wa kumi

Maoni katika picha
Tarehe mbili ya mwezi mtukufu wa Rajabu ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa mwezi ungáao, Imamu wa kumi mwenye utukufu mkubwa, Abu Hassan Ali Alhaadi mtoto wa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), alizaliwa pembeni ya mji wa Madina mwaka wa 212h, mama yake ni bibi mtukufu Sumana kutoka Moroko ajulikanae kwa nija la (Sayyidah) na huitwa Ummul-Fadhli, alikua anafunga siku zoto, hakua na mfano katika zuhudi na uchamungu.

Imamu Jawaad (a.s) alimpokea mwanae kwa furaha na shangwe kisha akamuweka kifuani kwake na akambusu na kumuadhinia kwenye sikio la kulia na akamsomea iqaama kwenye sikio la kushoto, baada ya hapo akampa jina alilokua kisha pewa mbinguni la (Ali) na akampa jina la kuniya la (Abu Hassan), kufuatia jina la babu yake Abu Hassan kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), kwa ajili ya kutofautisha kati yake na Abu Hassan kiongozi wa waumini na Abu Hassan Ridhwa (a.s) kwenye kuniya yake ikaongezwa (tatu), anaitwa Ali Alhaadi Abu Hassan wa tatu.

Miongoni mwa majila yake ya laqabu (sifa) ni: Najibu, Murtadhwa, Haadi, Naqiyyu, Aalimu, Faqiihi, Amiinu Mu-utamanu, Twayyibu na Mutawakkilu.

Alichukua madaraka ya Uimamu baada ya kufariki baba yake Imamu Jawaad (a.s), zama zake za Uimamu zilienda sambamba na zama za ukhalifa wa Mu’taswimu, Waathiqu, Mutawakkilu, Muntaswiru, Mustainu na Mu’tazu, alipambana na mambo mengi sana kutoka kwa makhalifa hao ambayo nafasi haitoshi kuyaeleza.

Wanahistoria wameandika kuwa Imamu (a.s) alikua kinara asiye fananishwa na yeyote katika zama zake, Shekh Tusi ameandika katika kitabu chake cha (Rijalu Tusi) majina ya wanachuoni mia moja na hamsini na nane waliosoma kwake, alikua ni marejeo ya wasomi wa fiqhi na sheria, vikaandikwa vitabu vya hadithi, mijadala, fiqhi, tafsiri kutokana na elimu yake na maarifa yake.

Ibun Shahari Aashubu anasema: Alikua mtu mwema zaidi na mfasaha wa kuongea, mwenye bashasha akiwa karibu na mkamilifu akiwa mbali, akinyamaza hupambwa na haiba nzuri ya unyenyekevu, na akiongea hupendeza, Hamadu Dini Hambaliy anasema: Alikua Faqihi, Imamu Mchamungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: