Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza shingano la (Ajru Risaalah) la filamu fupi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano la (Ajru Risaalah) la filamu fupi awamu ya kwanza, zinazofundisha misingi ya ubinaadamu inayo fundishwa na uislamu na malengo matukufu ya mafundisho ya Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) na kusahihisha picha mbaya inayopewa uislamu, shindano hili ni la kutengeneza video fupi zinye ujumbe tajwa na kujenga uaminifu baina ya watu wa Dini tofauti.

Makundi yanayo husishwa katika shindano hili ni:

Kwanza: watumishi wote wa Ataba tukufu.

Pili: watengenezaji wa filamu fupi kutoka mikoa yote ya Iraq, waigizaji na watunzi.

Masharti ya shindano na vigezo vyake

 1. Maudhui izungumzie uzuri wa uislamu na misingi ya ubinaadamu iliyopo katika mafundisho ya Mtume mtukufu na Ahlulbait wake (a.s).
 2. Isizidi muda wa takika (3).
 3. Mshiriki anahaki ya kuwasilisha zaidi ya kazi moja.
 4. Kazi iwe imetengenezwa rasmi kwa ajili ya shindano hili na haijawahi kushiriki kwenye shindano lingine, wala haijawahi kuonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii au mahala pengine popote.
 5. Utaangaliwa umakini wa kazi na itokane na vyanzo sahihi.
 6. Kazi (filamu) itengenezwe kwa lugha ya kiarabu, au kwa lugha yeyote ya kigeni lakini itafsiriwe kwa kiarabu.
 7. Mtoaji wa kazi (filamu) athibitishe kuwa anamiliki haki zote, pia anahaki ya kukabidhi filamu hiyo kwenye shindano hili.
 8. Kazi (filamu) isihusike na kutangaza huduma yeyote au kutangaza biashara.
 9. Kazi zitapokelewa zikiwa kwenye cd au flashi na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya au itumwe kwa njia ya mtandao kupitia link ifuatayo https://alkafeel.net/award/
 10. Kazi zitaanza kupokelewa tarehe 1 April 2021m hadi tarehe 15 April 2021m, matokeo ya shindano yatatangazwa siku ya kwanza ya sikukuu tukufu ya Iddi-Fitri.
 11. Haki zote za video hizo zitakuwa za Atabatu Abbasiyya tukufu, itakua na mamlaka ya kuzitumia itakavyo na mtayarishaji hana haki ya kurejeshewa filamu yake sawa awe amefaulu au hajafaulu.

Majaji na hatua za kutangaza walioshinda:

Kazi zote zitawasilishwa kwa kamati ya majaji itakayo teuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, nao watakua na mfumo kamili wa kushindanisha filamu hizo.

Zawadi:

Kwanza: hatua ya kwanza: waigizaji

 1. Mshindi wa kwanza atapewa dinari (1,500,000).
 2. Mshindi wa pili atapewa dinari (1,000,000).
 3. Mshindi wa tatu atapewa dinari (750,000).

Pili: sehemu ya pili: watunzi

 1. Mshindi wa kwanza atapewa dinari (750,000).
 2. Mshindi wa pili atapewa dinari (500,000).
 3. Mshindi wa tatu atapewa dinari (250,000).

 • Zingatia:

Zawadi ya mshindi wa kwanza haitatolewa kwa washindi wa sehemu ya kwanza na yapili kama kutakua hakuna filamu itakayo kamilisha vigezo.

Kwa maelezo zaidi tembelea mtandao wa Alkafeel kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/award/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: