Kituo cha utamaduni cha maelekezo na maendeleo kinafanya hafla ya kupongeza vijana wanao fikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria katika wilaya ya Sanjaar

Kituo cha utamaduni na maendeleo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambacho makao makuu yake yapo katika wilaya ya Sanjaar, kinafanya hafla ya kupongeza vijana wanaofikia umri wa kuwajibikiwa na sheria, sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Maimamu watakatifu (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (mabinti wa Mtume ni mabinti wa familia).

Kuhusu hafla hiyo tumeongea na msimamizi wa kituo hicho Shekh Haidari Aáridhwi amesema kuwa: “Tangu kuanzishwa kituo hiki na baada ya kukombolewa ardhi ya Sanjaar iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, kimefanya harakati nyingi, ikiwa ni pamoja na kufanya mahafali za usomaji wa Quráni na semina za kielimu, na kufanya vikao vya kuomboleza na kuadhimisha kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ikiwa ni pamoja na kuendesha mihadhara, nadwa na warsha mbalimbali, miongoni mwa harakati hizo ni hafla hii ya kuwapongeza mabinti wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya hafla hii imehusha ujumbe wa mkuu wa kituo Sayyid Mahmuud Aáraji, amesema kuwa hafla hii inalenga kuwajulisha mabinti umuhimu wa hatua wanayo ingia katika umri wao, na kuwajulisha majukumu yao na wajibu wao kisheria, sambamba na kuwakumbusha baadhi ya hadithi za Mtume na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) zinazo himiza uvaaji wa hijabu, na kumfanya bibi Zaharaa (a.s) kuwa kiigizo chema katika maisha yao, pia tumegawa zawadi kwa washiriki”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika hafla imepata matokea chanya na imejenga furaha kubwa kwa mabinti hao na wazazi wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: