Mwezi tatu Rajabu ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa kumi miongoni mwa Maimamu watakatifu wa nyumba ya Mtume Imamu Haadi (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi tatu Rajabu ni siku ya kukumbuka kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), Imamu wa kumi katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s), waliotajwa na Mtume (s.a.w.w).

Imamu Haadi alifia katika mji wa Samaraa mwaka wa (254h), Allamah Majlisi (r.a) amepokea kuwa Imamu Ali Haadi (a.s) alikufa kwa sumu akiwa na umri wa miaka arubaini na inasemekana alikua na miaka arubaini na moja, muuwaji wake (a.s) alikua ni Muútamad Abbasi, kama alivyo taja ibun Baabawaihi na wengineo, na inasemekana kuwa muuwaji wake alikua ni Muútazu Abbasi.

Imamu Haadi (a.s) aliishi katika mji wa Madina miaka ishirini, baada ya hapo Mutawakilu Abbasi akamtaka aende katika mji wa Samaraa, akaishi huko miaka ishirini hadi alipo uwawa kwa sumu, na akazikwa nyumbani kwake sehemu ambayo kaburi lake lipo hadi sasa, baada ya kukaa gerezani kwa muda mrefu.

Masudi anasema katika kitabu cha (Ithbaatu-Waswiyyah), Abu Hassan alipo ugua maradhi ya kifo chake aliingia Abu Muhammad (a.s) na akamhusia.

Akasema pia: Alipofariki (a.s) bani Hashi wote/ Twalibiyyina na Abbasiyyina walikusanyika ndani ya nyumba yake pamoja na kundi kubwa la wafuasi wake, kisha ukafunguliwa mlango wa korido na akatoka mtumishi aliyekua ni mtu mweusi, kisha baada yake akatoka Abu Muhammad Hassan Askariy (a.s) akiwa kichwa wazi na amevaa nguo iliyo chanika, alikua anafanana sana na baba yake (a.s), walikuwepo pia watoto wa Mutawakilu na baadhi yao wakiwa ni viongozi wa ahadi (Ulaatu-Ahdi), hakubaki mtu hata mmoja ispokua alisimama.

Akakaa (a.s) katikati ya milango miwili ya korido huku watu wote wakiwa mbele yake, nyumba ilikua na kelele kama sokoni kutokana na mazungumzo ya watu, lakini alipotoka (a.s) na kukaa watu wote wakakaa kimya, haikusikika sauti ispokua ya chafya, kisha yule mtumishi akasimama pembeni ya Abu Muhammad (a.s), halafu wakatoa jeneza pamoja naye (a.s) wakatembea hadi barabarani, Abu Muhammad (a.s) alikua amesha liswalia kabla ya kutolewa kwa watu, na lilipo tolewa Muútamadi akaliswalia, kisha akazikwa katika moja ya nyumba zake, siku hiyo ulisikika ukulele katika mji wa Samaraa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: