Asubuhi ya Jumanne mwezi (3 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (16 Februali 2021m), maukibu ya kuomboleza ya watu wa Karbala imeelekea kwenye haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoa pole ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), na imekua maukibu ya kwanza kuomboleza msiba huo mkubwa unao umiza nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) aliye kufa siku kama ya leo, wameomboleza kupitia mkusanyiko mkubwa kama walivyo zowea kufanya kila kwenye tukio la msiba.
Kama desturi ya kuomboleza, matembezi yao yameanzia kwenye moja ya barabara iliyo elekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi kwenye haram yake takatifu wakiwa wamebeba jeneza la igizo, baada ya hapo wakaelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram hiyo, wakati wa matembezi waombolezaji walikua wamesimama kwa mistari, huku wakiimba qaswida za huzuni na majonzi, zilizo taja yaliyojiri kwa Imamu (a.s), na namna alivyo tengwa na wafuasi wake.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kuomboleza msiba huu ni sehemu ya matukio yaliyo zoweleka kufanywa na maukibu hii, Ataba mbili zimejitolea kila kitu kilicho hitajika kuwezesha matembezi ya maukibu hiyo, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, sambamba na kuandaa njia ya maukibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, hii sio mara ya kwanza bali hufanywa hivi kwenye kila tukio ndani ya mwaka mzima”.