Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Haadi (a.s)

Maoni katika picha
Kutokana na kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amhuishe atakae huisha mambo yetu), majlisi ya kuomboleza imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kuhuisha kifo cha Imamu wa kumi katika maimamu wa Ahlulbait (a.s) Imamu Haadi (a.s), ambaye tarehe ya kifo chake inasadifu siku kama ya leo mwezi (3 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (16 Februali 2021h), na kuhudhuriwa na watumishi wake wakiwa wamechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.

Mhadhiri wa majlisi hiyo alikua ni Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameeleza historia ya Imamu Haadi (a.s) kufuatia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho), ameongea mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:

  • - Mifano ya maudhi ya Abbasiyyina kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao pamoja na wafuasi wao, na namna siasa yao ilivyo kua dhidi wa Ahlulbait (a.s) baada ya kujua nafasi yao kidini na kijamii, walikua hawajipendekezi kwa watawala na wafalme, walikua watu wa msimamo na misingi ya Dini, kama ilivyo kua kwa Imamu Haadi (a.s).
  • - Aliyofanya Mutawakilu Abbasi kwa Imamu Haadi (a.s), kumfunga na kumuweka kizuwizini katika maeneo tofauti, na namna alivyo fuatilia harakati zote za Imamu (a.s) ndani na nje ya nyumba yake.
  • - Njia na nyenzo walizotumia watawala wa bani Abbasi walio ishi katika zama za Imamu Haadi (a.s) za kuwatesa na kuwanyanyasa wapenzi na wafuasi wa Imamu (a.s).
  • - Karama za Imamu Haadi (a.s) na miujiza aliyopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu.
  • - Namna alivyo fanikiwa Imamu (a.s) kufikisha ujumbe wa baba zake na babu zake, ujumbe aliokuja nao babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Maimamu baada yake.

Akahitimisha mhadhara kwa kusoma tenzi kuhusu msiba huu mkubwa na huzuni kubwa iliyopo katika nyoyo za waislamu, watu wote walio hudhuria wakajaa huzuni kubwa na majonzi kutokana na msiba huu adhim baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: