Kuomboleza kifo cha Imamu Haadi (a.s): Zinafanyika majlisi za kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), ambazo ni sehemu ya ratiba ya uombolezaji iliyopangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika tukio hili adhimu, majlisi zitaendelea kwa muda wa siku tatu kuanzia jana mwezi pili Rajabu hadi mwezi nne, kila siku zinafanywa majlisi mbili, asubuhi na jioni, pamoja na kufanya tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.

Yameelezwa haya na kiongozi wa idara hiyo Shekh Abdu-Swahibu Twaiy, akaongeza kuwa: “Majlisi zinafanywa chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), unaohusika na uratibu na ufanyaji wa harakati tofauti ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka, mwaka huu tumeamua kufanya majlisi mara mbili: asubuhi amealikwa mhadhiri Shekh Jaasim Haatamiy, na jioni mhadhiri ni Shekh Raádu Khatwibu, pamoja na kufanya majlisi ya maatam”.

Akaendelea kusema: “Mawaidha yanayo tolewa na wahadhiri hao yanahusu historia na mwenendo wa Imamu Haadi (a.s), kila mhadhiri mada yake inatofautiana na mwenzake, wameongelea nyanja mbalimbali za maisha ya Imamu Haadi (a.s), na changamoto alizo pitia katika uhai wake kutoka kwa watawala wa zama zake, na namna alivyo weza kufundisha misingi ya uislamu halisi na mwenendo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) pamoja na changamoto zote alizo pitia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: