Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Haadi (a.s): chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya majlisi ya kuomboleza

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa kumi miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) Ali Naqii Alhaadi (a.s), katika ukumbi wa Abul-Aswadu Du-Uliyyu ndani ya chuo hicho, na kuhudhuriwa na walimu, watumishi na wanafunzi, wakiongozwa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani.

Majlisi imefunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Hafidhu Dujaili, akazungumzia maisha ya Imamu Haadi (a.s), na namna alivyo sambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) pamoja na dhulma aliyofanyiwa, na mambo mengine aliyo fanyiwa na watawala wa bani Abbasi, akabainisha kuwa Imamu (a.s) alikua na nafasi muhimu katika zama hizo, alisimamia misingi sahihi ya Dini tukufu ya kiislamu na mwenendo sahihi wa Ahlulbait (a.s) pamoja na changamoto nyingi alizo pambana nazo yeye na wafuasi wake.

Majlisi ikahitimishwa kwa utenzi wa huzuni kuhusi kisa cha kifo chake (a.s), uliotaja dhulma alizo fanyiwa wakati wa uhai wake na wakati wa kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: