Kuratibu opresheni ya kutambua mapema virusi vya Korona

Maoni katika picha
Idara ya mambo ya kitabibu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala, inaratibu opresheni ya utambuzi wa haraka wa virusi vya Korona, kwa watu wanaotaka kufanya ziara kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuweka vituo vya upimaji katika milango mikuu ya kuingia ndani ya haram tukufu chini ya usimamizi wa madaktari mahiri na wauguzi hodari.

Tumeongea na mmoja wa wasimamizi wa opresheni hiyo kutoka idara ya tiba Siyyid Aadil Saadi Jihadi amesema kuwa: “Kutokana na kuongezeka maambukizi ya virusi vya Korona tumechukua tahadhari zaidi za kujikinga na maambukizi, ili kulinda afya na usalama wa mazuwaru na kuepusha maambukizi baina yao, tumeamua kuweka vituo vya upimaji kwenye milango mitatu mikubwa ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mlango wa Kibla na mlango wa Imamu Jawadi na Imamu Mussa Alkaadhim (a.s), kila sehemu ya mlango katika milango hiyo tumeweka vifaa-tiba vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya upimaji, tunafanya kazi hii kwa kushirikiana na wataalamu kutoka idara ya afya ya mkoa wa Karbala pamoja na jopo la wataalamu wa kujitolea”.

Akaongeza kuwa: “Wataalamu hao wanafanya kazi kwa haraka, wamechukua sampo (5000) kwa mara ya kwanza, iwapo akipatikana mtu mwenye maambukizi atatunzwa sehemu maalum iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kisha hatua zingine zitafuata”.

Akasisitiza kuwa: “Vituo hivyo haviishii kwenye kuchukua sampo na kupima Korona peke yake, bali vinapima pia sukari na maradhi mengine pamoja na kutoa matibabu yanayo hitajika, sambamba na kutoa maelekezo ya namna ya kuamiliana na mtu aliye ambukizwa virusi vya Korona na kuhimiza kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi, kama vile kuvaa barakoa na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua tahadhari zaidi ya kujikinga na maambukizi tofauti na ilivyokua awali, kama vile kugawa barakoa na vitakasa mikono kwa mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: