Toleo la (tatu na nne) la jarida la turathi za Karbala

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa toleo la tatu na nne/ katika juzuu la saba/ mwaka wa saba, la jarida la turathi za Karbala.

Rais wa wahariri wa jarida Dokta Ihsani Ghuraifi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Toleo hili limekusanya mada za kielimu za aina mbalimbali, zimeandikwa na wasomi kutoka ndani na nje ya Iraq, miongoni mwa mada hizo ni:

  • - Sayyid Muhammad Haadi Milaani, ameandika kuhusu utaratibu wa kuthibitisha fadhila na hoja kutoka katika kitabu cha (tutawatambua vipi viongozi wetu).. kilicho andikwa na Murtadha Sayyid Haidari Sharafu-Dini Mussawi.
  • - Dondoo za historia ya Shekh Haadi Karbalai aliye fariki mwaka (1412h) imeandikwa na Shekh Alaa Karbalai/ kutoka hauza ya Karbala tukufu.
  • - Muhtasari wa faharasi kutoka katika kitabu cha Muntakhabu-Dini kilicho andikwa na Kafámiy.. utafiti na uhakiki, umeandikwa na Dokta Ali Twaahir Alhilliy/ kutoka chuo kikuu cha Karbala.
  • - Ruuhu-Llah Swiyadi Najadi/ kutoka chuo kikuu cha Kashani Iran, imeandikwa na mtafiti wa uchumi katika mji wa Karbala hadi mwaka 1918m, Intiswaru Abdu-Aun Muhsin Saadi kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya.

Kumbuka kuwa jarida la turathi za Karbala ni miongoni mwa majarida bora ya kielimu yanayo tolewa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na vituo vya tafiti, linaendelea kutolewa na kutuo cha turathi za Karbala kwa mwaka wa saba mfululizo, linakubaliwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu katika taifa la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: