Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad inafanya nadwa chini ya anuani isemayo (Ishara katika Quráni tukufu)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdadi chini ya Atabatu Abbasiyya imefanya nadwa ya Quráni yenye anuani isemayo: (Ishara katika Quráni tukufu), ikiwa ni sehemu ya nadwa zinazo fanywa na Maahadi katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine, chini ya wahadhiri wa hauza na walimu wa sekula.

Miongoni mwa waliowasilisha mada katika nadwa hiyo ni Ustadh Majidi Ma‎ayufi, ameongea mambo mengi kuhusu maana na uwelewa wa Quráni na kutafakari katika aya takatifu za Quráni, nadwa hiyo imehudhuriwa na kundi kubwa la wanafunzi na wadau wa Quráni.

Tambua kuwa nadwa imefanywa katika kitongoji cha Karkhi, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni sekta muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya kazi ya kueneza mafundisho ya Quráni na kuandaa kizazi kunacho fanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: