Kikosi cha Abbasi kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wanaendesha opresheni ya kupuliza dawa kwenye mikoa tofauti ya Iraq, hivi karibuni wameendesha opresheni hiyo katika mkoa wa Baabil iliyo husisha maeneo tofauti.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Ofisi yetu katika mji wa Baabil imepokea maombi ya kupuliza dawa kutoka taasisi za serikali za afya na elimu, kutokana na maombi hayo tumeratibu kazi ya kupuliza dawa kwenye vituo vya afya na mashuleni, kuanzia kituo cha afya cha Ali bun Muhammad Samriy na kituo cha Abdullahi bun Zaidi Shahidi na shule ya msingi mchanganyiko.

Akaongeza kuwa: kazi hii inafanywa chini ya maelekezo ya uongozi wa kikosi, kwa lengo la kulinda afya za wananchi na wanafunzi watukufu, tutaendelea na kazi hii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hadi tatizo la virusi vya Korona litakapo isha katika mkoa wa Baabil.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kimesha fanya kazi ya kupuliza dawa katika miji mingi hasa yenye wakazi wengi, na inafanya kila iwezalo katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, kamati hiyo pia imejenga kituo katika mkoa wa Karbala cha kuosha na kuzika watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: