Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanya upasuaji wa moyo (366) kwa watu wazima na kufanikiwa asilimia %98.90

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamesema kuwa wamefanya upasuaji wa moyo kwa watu wazima na kufanikiwa asilimia (%98.90), inachuana na mafanikio ambayo hupatikana katika hospitali kubwa za maradhi ya moyo duniani.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo Dokta Bashiri Akbinaar amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu ndani ya miaka mitano ya kufanya kazi katika hospitali ya rufaa Alkafeel mkoani Karbala, wamefanya upasuaji (366) wa moyo kutoka mikoa tofauti ya Iraq”.

Akabainisha kuwa: “Kiwango cha mafanikio kilicho patikana katika upasuaji huo kimefika asilimia (%98.90), hiki ni kiwango cha juu katika sekta ya upasuaji wa moyo, kwa asilimia hiyo hospitali yetu inachuana na hospitali kubwa za moyo katika eneo sawa ziwe za Uturuki au nchi zingine”.

Akaongeza kuwa: “Jambo kubwa lililo saidia kupatikana kwa mafanikio hayo, ni mazingira bora ya kazi na vifaa-tiba vya kisasa pamoja na madaktari bingwa na wauguzi mahiri waliopo”.

Akasema: “Asilimia kubwa ya upasuaji uliofanyika ulikua mkubwa na ulihitaji uwezo maalum na vifaa vya kisasa, pamoja na uangalizi wa karibu baada ya upasuaji, yote hayo yanapatikana vizuri katika hospitali ya rufaa Alkafeel”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa fani mbalimbali kila baaada ya muda, pamoja na kupokea wagonjwa walio katika hatua tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: