Atabatu Abbasiyya tukufu imeipa vitabu maktaba ya chuo kikuu cha ulinzi

Maoni katika picha
Maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekipa vitabu chuo kikuu cha Ulinzi, chuo cha kijeshi kilicho chini ya wizara ya ulinzi ya Iraq, kwa ajili ya kusaidia kuboresha maktaba na kuinua kiwango cha hazina ya elimu, kwa ajili ya kuhudumia wasomi na watafiti wa mambo ya vita na ulinzi katika chuo hicho.

Vitabu hivyo vimekabidhiwa kupitia mkuu wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma Ustadh Hasanain Mussawi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Vitabu hivi vimetolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kusaidia maktaba za serikali na binafsi, jambo ambalo linasaidia sekta ya utafiti wa kielimu, na kuimarisha uhusiano wa kielimu hakika zaka ya elimu ni kuisambaza, jumla ya aina (83) ya vitabu tofauti vya dini, historia na mikakati ya kimataifa vimetolewa”.

Ugeni huo umepokelewa na rais wa chuo Jenerali Saadi Muzharu Alaaq, ametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya na watumishi wake kwa kutoa vitabu hivi, akasema kuwa: “Vitabu hivi kuongezwa katika maktaba vinaimarisha nafasi ya maktaba na kuwa sehemu muhimu ya kurejea katika mambo ya kitamaduni na vitabu mbalimbali”.

Akasifu nafasi kubwa waliyo nayo Atabatu Abbasiyya na uwepo wake endelevu katika jamii ya raia wa Iraq kwenye mambo ya elimu na utamaduni, akasema kuwa chuo kipo tayali kuendelea kushirikiana na Ataba kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wake katika maswala ya elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: